Mpira wa miguu una mambo mengi tena mara nyingine unaweza kushangazwa zaidi na mambo ya ajabu yanayotokea viwanjani na kulazimika mechi kusimama kwa muda. Hutokea wachezaji wakiwa wanapambana kuzitafutia ushindi timu zao jambo lisilotegemewa kutokea na kuwaacha wachezaji wameduwaa.

Leo nimekuandalia List ya mambo tano yasiyo ya kawaida yaliyosababisha mechi kusimama kwa muda, Unaweza itazama kwa Mfumo wa Video na Sauti hapa Chini.

https://youtu.be/A-Uc3FnXVDc

Sasa Twende Kazi kwa kuanza na Jambo la Tano.

5. Ndege Zisizo na Rubani (Drone)

Mwezi  wa kumi wa mwaka 2015 katika mechi ya kufuzu kushiriki michuano ya EURO kati ya Serbia na Albania ililazimika kusimama kwa muda kabla ya half time. Katika dakika ya 41 ya mchezo kitu kisichotegemewa kutoka angani kilishuka huku kikiwaacha midomo wazi wachezaji na mashabiki pia. Mwanzo alidhaniwa kuwa ni ndege wa porini lakini hakuwa ndege isipokuwa ilikuwa ni Drone iliyokuwa imefungwa bendera ya Taifa ya Albania. Hali hiyo iliamsha hisia kali kati ya Nchi hizo mbili kutokana na maelewano yao kisiasa kuwa sio mazuri. Kitendo hicho kilipelekea UEFA kuzichunguza Nchi hizo kwani kitendo hicho kilitafsiliwa kama kuleta siasa katika mpira.

4. Paka Mweusi

Kuna wanaoamini kuwa paka mweusi ni ishara ya bahati mbaya, katika mechi kati ya Heracles na FC Groningen alitokea paka uwanjani na refa kulazimika kusimamisha mchezo hadi paka huyo aondoke. Alifukuzwa na baadae alikamatwa na kutolewa nje ya uwanja. Tukio hili lilishangaza wengi kutokana na watu kuwahusisha paka wa aina hiyo na imani za kishirikina.

3. Selfie

Moja kati ya mambo ya kushangaza kabisa katika mpira wa miguu ni tukio lililokatokea katika uwanja wa Tottenham Hotspur unaojulikana kwa White Hart Lane. Tukio hilo la aina yake lilitokea katika mechi ya UEFA Europa League kati ya Spurs na Partizan Belgrade. Mchezo ulisimamishwa baada ya mashabiki watatu kuingia uwanjani kila mmoja akikimbilia upande wake. Walivamia uwanja wakiwa wamevaa T-shirts zilizoandikwa “BassBuds” kampuni inayojulikana kwa kutengeneza Headphone. Mashabiki wote watatu waliingia uwanjani na kwenda waliposimama wachezaji watatu wa Tottenham na kuanza kupiga hizo Selfie lakini waliondoshwa na walinzi wa uwanjani hapo. Tukio hilo lilipoteza takribani dakika 10.

2. Kijana Mdogo Wa Kiume

Hili tukio la Mtoto kuingia uwanjani lilitokea miaka ya 1970 katika uwanja wa Machester United Old Trafford ambapo Man Utd walikuwa wanacheza. Wakati krosi imepigwa kutoka upande wa kulia mwa uwanja na kupigwa kichwa, kijana mmoja alitokea uwanjani na kupiga shuti kali. Licha ya kuwa hakulenga lango na kufunga goli lakini tukio hilo limekuwa ni kituko kikali zaidi kuwahi kutokea katika mpira wa Miguu.
Tukio kama hilo lilitokea pia hivi karibuni nchini South Africa Brazil iliposhinda magoli 5 – 0 ambapo kijana mdogo aliingia uwanjani, lakini tofauti na huyo wa mwanzo yeye alifurahiwa na wachezaji na kunyanyuliwa juu.

1. Kuku

Huko Ureno kuku aliingia uwanjani wakati Benifica wakicheza na wapinzani wao wakubwa FC Porto, mechi ilibidi isimame ili kuku huyo aweze kuondolewa. Palitokea patashika walinzi wa hapo kiwanjani wakikimbia huku na kule kumfukuza kuku huyo. Ikabidi mashabiki waambiwe kuwa kwa atakaeweza kumshika kuku huyo basi angepewa zawadi ndipo vurugu zikaongezeka. Mechi hiyo ilimalizika kwa Benifica kupokea kichapo cha magoli 5 – 0 dhidi ya Porto.

TUMEKUANDALIA MAKALA HII KWA MFUMO WA VIDEO NA SAUTI, ITAZAME HAPA

https://youtu.be/A-Uc3FnXVDc

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here