HIVI HAPA VIPIGO VIKUBWA ZAIDI KWENYE, LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Moja kati ya shindano kubwa Afrika ni shindano ambalo linawakutanisha mabingwa katika ligi kutoka kwenye nchi zilizomo katika bara hili ambalo linaitwa CAF Champions League “CAFCL” ambapo shindano hili lilianzishwa mwaka 1964 likiwa linaitwa African Cup of Champions Clubs kabla ya mwaka 1997 kubadilishwa na kuitwa kama inavyoitwa sasa CAF Champions League.
Miaka ya hivi karibuni Timu za Tanzania zimekuwa zikijaribu kufanya vizuri katika ligi hiyo na kujitengenezea heshima na hii ikianza na Simba SC ambaye ameshiriki katika misimu mitano na kutengeneza katika timu pekee ambazo zimeingia katika hatua ya Robo fainali kwa misimu mitano mfululizo.
Msimu uliopita nao Yanga SC wakifanya vizuri katika shirikisho Afrika huku kwa msimu wa 2023/2024 wakifanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali baada ya miaka 26 kupita na hiyo kufanya kuwa Tanzania iwe nchi pekee ambayo ina timu mbili ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua ya Robo Fainali.
Katika kipindi chote hicho leo tumekuletea timu ambazo ziliwahi kutoa vipigo vikubwa katika Klabu bingwa Afrika na hata zile zilizowahi kupoke vipigo hivyo ambapo imebakia historia katika makabati ya CAF.
Hizi hapa Timu zilizowahi kutoa vipigo vikubwa CAF
- 2019: TP Mazembe 8-0 Club Africain
- 2023: Simba SC 7-0 Horoya AC
- 2001: ASEC Mimosas 7-0 CR Belouizdad
- 1998: Raja CA 6-0 Young Africans
- 2004: Enyimba FC 6-0 Big Bullets
- 2024: Simba SC 8-0 Galaxy FC