KOCHA wa Yanga Miguel Gamondi amesema timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyopangwa kucheza na Yanga hatua ya robo fainali na timu ya Aly Ahly ya Misri iliyopangwa kucheza na Simba hatua hiyo zinapaswa kucheza fainali kwa kuwa ni timu kubwa na zenye uzoefu wa mashindano hayo na pia zina uwekezaji mkubwa wa kifedha.
Amesema Mamelodi wana uchumi mkubwa akitolea mfano kwenye dirisha dogo Mamelodi wamenunua mchezaji kutoka Argentina kwa fedha nyingi wakati Yanga imewasajili Guede na Okra kwa gharama za kawaida tofauti na Mamelodi.
Akizungumzia kuhusu kushindana na Mamelodi, kocha huyo amesema kwa kuwa watakuwa wachezaji 11 kwa 11 watapambana kusaka ushindi bila kujali uwezo wao wa kifedha ama uzoefu wao katika mashindano makubwa ingawa amesema changamoto kubwa aliyoioana kwa wachezaji wengi wa Tanzania wamekosa uzoefu wa mashindano makubwa.