BAADA ya kuondolewa katika Mapnduzi 2024 katika hatua ya robo fainali dhidi ya Simba, Singida Fountain Gate wameweka shida chini na kuwapa ruhusa wachezaji kula bata kwa mapumziko mafupi.

Ipo wazi kuwa Januari 10 ubao ulisoma Singida Fountain Gate 1-1 Simba kwenye penalti ilikuwa Singida Fountain Gate 2-3 Simba na timu hiyo ikagotea hatua ya robo fainali.

Kwenye Mapinduzi 2024 Singida Fountain Gate ilikutana mara mbili na Simba na ilipoteza mechi zote mbili ndani ya dakika 180, hatua ya makundi ubao ulisoma Simba 2-0 Singida Fountain Gate.

Ofsa Habari wa Singida Fountain Gate Hussein Masanza amesema kuwa walialikwa kwenye Mapinduzi wanashukuru kwa yote wanajipanga kwa wakati ujao.

“Baada ya kualikwa kwenye Mapinduzi timu tunashukuru kwa yote yaliyotokea ambapo wachezaji wetu wamepatiwa mapumziko ya muda wa wiki mbili ili kurejea kwenye ubora wao.

“Ni kuanzia Januari  12 Januari 2024 mapumziko yao yanaanza mpaka wiki mbili zikiisha, watarejea kambini Januari 27 kwa maandalizi ya mechi zetu za Ligi Kuu Bara,” amesema Masanza.

Januari 13 ilipigwa fainali Uwanja wa New Aman Complex ni Mlandege walishinda bao 1-0 huku Elvis Rupia wa Singida Fountain Gate akiwa ni mfungaji bora baada ya kufunga mabao matano.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here