HUKU wengi wakiipa nafasi zaidi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga Machi 30, mwaka huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ameichambua timu hiyo na kusema hakuna lisilowezekana kwa kuwa watakuwa 11 kwa 11 uwanjani na si vinginevyo.
Akiwachambua wapinzani wao hao, Gamondi amesema ubora wa kikosi na bajeti ya usajili wa Mamelodi Sundowns tofauti na Yanga, lakini hilo haliwapi woga, badala yake wanahitaji kupambana na kuweka juhudi zaidi katika mchezo huo wa nyumbani.
Gamondi amesema anafahamu misingi ya Mamelodi kwa sababu timu yake ya zamani na wamekuwa bora sana kwa msimu huu, na kwamba waliongeza mchezaji kutoka Argentina kwa usajili ghali tofauti na wao ambao dirisha dogo waliwaleta Joseph Guede na Augustine Okrah wakiwa wachezaji huru.