MWENYEKITI wa Kamati ya Maboresho ya Katiba ya klabu ya Simba, Hussein Kitta amesema wanachama wamepitisha mambo sita ambayo walitakiwa kufanyia maboresho.

Mambo hayo ni mamlaka ya uteuzi ya bodi ya wadhamini baada ya kuteuliwa na sasa wanatakiwa kuchaguliwa katika mkutano mkuu, kuweka wazi nafasi ya kupatikana kwa Mwenyekiti, kuweka wazi malengo ya Katiba na kuyaweka wazi malengo ya mkutano

Kuwa na haja ya kuwa na kupitisha Kampuni ya inayoshiriki HISA za Simba Sport Club na kuweza wazi HISA asilimia 99 inashikiliwa na bodi ya wadhamini na asilimia moja kwa Mwenyekiti ambaye anatakiwa kuwa wazi kuwa ni wanachama na kipengele cha sita ni mwakilishi mmoja wa wanachama katika mkutano mkuu.

Kitta alisema wanachama wamekataa kupitisha kipengele kimoja kinachoeleza kutoa mwakilishi wa mwanachama katika mkutano mkuu.

“Hicho kipengele tuliambiwa tukiweke kulingana na namna ya kuendesha mikutano yetu, lakini wanachama wamekikataa, kutokana na hilo ni sehemu ya mapendekezo tu tuliopewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT ) ambayo haikuwa na ulazima,” alisema Kitta.

Naye Mjumbe wa bodi ya ushauri wa klabu ya Simba, Geofrey Kaburu amempongeza mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu kwa kuendesha mkutano vizuri na kufuata matakwa ya wanachama.

Alisema mkutano ulikuwa mfupi wenye ajenda nzuri zilizo na mafanikio kwa klabu huku akikisisitiza kuwa katiba inatambua mahitaji ya wanachama hivyo kupewa nafasi ya kusikilizwa ni jambo zuri.

“Pia Baraza letu limeingizwa kwenye katiba ya klabu hivyo tutakuwa tunashauri kwa mujibu wa katiba kwasababu tayari tunatambulika;

Mbali na sisi kutambulika kikatiba rasmi mwenyekiti wa klabu kapewa nafasi maalum kwa mujibu wa katiba kusimama kwaajili ya wanachama.” alisema Kaburu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here