UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa mpango mkubwa kwa sasa ni kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Timu hiyo imetinga hatua hiyo ikiwa nafasi ya pili kwenye kundi B na pointi zake ni 9 inatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Uwanja wa Mkapa.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mpango mkubwa kutinga hatua ya nusu fainali ni muhimu kupata matokeo dhidi ya Al Ahly katika robo fainali.
“Sasa tunaanza maandalizi rasmi ya mchezo wetu wa robo fainali dhidi ya Al Ahly. Kwenye Makundi yetu ya WhatsApp na matawi yetu tuanze kuhamasishana tujitokeze kwa wingi Uwanjani siku ya Machi 29.
“Wale wa mikoani tuanze sasa kukusanya nauli kwa ajili ya kuja Dar Es Salaam kushuhudia mchezo huo na kuipeleka Simba yetu nusu fainali.
“Kwa Wana Simba wote mjadala wetu mkubwa ndani ya wiki mbili hizi iwe ni kuujaza Uwanja wa Mkapa na mapambano ya kumuua Ahly. Ahly anatakiwa kufa kifo kibaya Benjamini Mkapa na hili wana Simba tunaliweza,”.