KITAIFA
BANYANA WAWASILI NCHINI KUKIPIGA NA TWIGA STARS
Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) tayari kimewasili nchini Tanzania kwaajili ya kucheza mchezo wa kutafuta kufuzu kucheza michuano ya Olimpiki ya 2024 dhidi ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars).
Mchezo huo utapigwa kesho Ijumaa majira ya saa 10 jioni katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.