WINGA Jesus Moloko nyota wa Yanga anatajwa kuwa kwenye hesabu za kupewa mkono wa asante.
Nyota huyo hajawa na nafasi kwenye kikosi cha Miguel Gamondi ndani ya Yanga kutokana na ushindani wa namba.
Alikuwa kwenye kikosi kilichoshiriki Mapinduzi 2024 kikagotea hatua ya robo fainali kwa kushuhudia ubao ukisoma Yanga 1-3 APR FC.
Raia huyo wa DR Congo ndani ya ligi hajapata zali la kufunga huku timu hiyo ikiwa imecheza jumla ya mechi 11 ikishinda 10 na kupoteza mchezo mmoja.