1. Uzoefu. Licha ya CS Sfaxien ya Tunisia kuwa bingwa mara tatu wa michuano hiyo, bado Simba inabaki kuwa timu yenye uzoefu mkubwa na mashindano ya CAF kwa miaka ya Karibuni. Uzoefu unaiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kufanya vizuri.
2. Usajili mkubwa. Msimu huu Simba imefanya usajili mkubwa wa nyota 14 ambao wameifanya kuwa imara zaidi ya mwaka jana. Wachezaji wenye uzoefu kama Leonel Ateba, Jean Ahoua, Moussa Camara, Debora Fernandez na wengineo wanaiweka Simba kwenye nafasi ya kufanya vizuri.
3. Kurejea kwa MO Dewji. Kurejea kwa Bilionea, Mohamed Dewji ‘MO’ kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kumeongeza nguvu, hamasa na morali ya kupambana ndani ya Simba. Siku zote Dewji Amekuwa akisisitiza lengo la kutwaa taji la Afrika hivyo msimu huu huenda akaweka nguvu kubwa zaidi ya kifedha Ili kufanya vizuri.
4. Nguvu ya Simba ugenini. Uwezo wa Simba kufanya vizuri kwenye mechi za ugenini umekua kwa kasi kubwa kwa kadri miaka inavyokwenda. Kwenye mechi za hatua ya Makundi mwaka Jana Simba ilipoteza mechi moja tu ugenini. Hivyo kwa namna Simba imekuwa ikifanya vizuri kwa Mkapa na ilivyoimarika ugenini ni wazi kuwa Ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri.
5. Nguvu ya Mashabiki. Afrika nzima inakiri kuwa Simba imekuwa na mashabiki wenye hamasa kubwa sana katika mechi za CAF pindi inapocheza nyumbani. Mashabiki wa Simba wamekuwa na imani kubwa na timu yao katika mashindano ya CAF na kuwa silaha muhimu ya timu hiyo kufanya vizuri.