TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU 12.08.2024
Arsenal wanapanga kumnunua winga wa Bayern Munich Kingsley Coman, mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney anafuatiliwa na vilabu vya Saudi Pro League, Newcastle United wanataka kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Nikita Parris.
Arsenal wanapanga kumsajili winga Mfaransa Kingsley Coman kwa mkopo kwa msimu huu, huku Bayern Munich wakiwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka. (Football Insider)
Mshambulizi wa Brentford Ivan Toney anaangaliwa na vilabu vya Saudi Pro League, huku Al-Ahli wakimtaka nyota huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 28. (Fabrizio Romano)
Newcastle United wanalenga kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Nikita Parris, 30, huku wakitarajia kupandishwa kwenye Ligi Kuu ya Wanawake.(Guardian),
Stuttgart wako kwenye mazungumzo ya kumsajili Armando Broja kwa mkopo kutoka Chelsea, huku mshambuliaji huyo wa Albania mwenye umri wa miaka 22 akiwa tayari kujiunga na klabu hiyo ya Ujerumani. (Sky Sports Ujerumani)
AC Milan wanataka kumnunua kwa mkopo na chaguo la kumnunua mshambuliaji wa Roma Mwingereza Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 26, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bournemouth, Everton na Leicester City.(Calciomercato – Kiitaliano)
Nottingham Forest imekataa ombi la Atalanta la zaidi ya €20m (£17.1m) kumnunua beki wa Wales Neco Williams, 23. (Fabrizio Romano)
Beki wa Liverpool Virgil van Dijk amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Reds na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 33, anasema hakuna mabadiliko yoyote katika hali ya mkataba wake. (Liverpool Echo)
Kipa wa Brazil Ederson, mwenye umri wa miaka 30, amekuwa akihusishwa na kuhamia Saudi Arabia lakini anasema anasalia Manchester City baada ya mazungumzo na meneja Pep Guardiola(Mirror),
Leicester City wametuma dau la pauni milioni 23.2 kumnunua mshambuliaji wa Panathinaikos na Ugiriki Fotis Loannidis mwenye umri wa miaka 24 huku wakiendelea na mazungumzo ya kujaribu kumnunua winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 31, kutoka Galatasaray. (Telegraph – usajili unahitajika)
Brentford wamekubali dili la kumsajili kiungo wa kati wa Sweden Jens Cajuste kutoka Napoli kwa mkopo wa msimu mzima, naahadi ya kumnunua kwa takriban £10m. (Football Insider)
Borussia Dortmund wanatazamia kumsajili fowadi wa Ujerumani Maximilian Beier, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Hoffenheim kwa mkataba wa thamani ya zaidi ya €30m (£25.7m). (Sky Sports Ujerumani)