Daktari wa klabu ya Simba Edwin Kagabo amethibitisha kuwa kiungo mshambuliaji Joshua Mutale raia wa Zambia atakuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza jeraha alilolipata kwenye mchezo wa kwanza wa ligi.
Mutale alipata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United uliopigwa katika Uwanja wa KMC jumapili iliyopita ya Agosti 18.
Dkt. Kagabo amesema Mutale hajapata majeraha makubwa lakini ili kumlinda asiumie zaidi atakuwa nje ya uwanja kwa muda huo.