WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Azam FC wameweka wazi kuwa licha ya kupata ushindi katika mchezo wa mkondo wa kwanza bado hawana furaha.
Matajiri hao wa Dar Azam FC, Agosti 18 2024 walikuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya APR ya Rwanda na wakaibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa kipindi cha pili baada ya dakika 45 za mwanzo wote kutofungana na mtupiaji ni Blanco ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti iliyosababishwa na kiungo mshambuliaji Fei Toto.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC kupitia ukurasa wake wa Instagram amedondosha ujumbe huu mara baada ya mchezo kugota mwisho: Tumeshinda Ndio lakini hatuna Furaha. Kwanini kwa sababu tuna timu imara ambayo inapaswa kuwa bora zaidi ya pale.
“Wakati mwingine ili kupona lazima kunywa dawa chungu, tunahitaji kuimarika zaidi wachezaji na benchi la ufundi mashabiki wanawategemea tunahitaji kukua kifikira zaidi ya pale Azam sio timu ya daraja la leo.
“Otherwise tumeshinda mchezo mgumu tunahitaji kuutunza huu ushindi na uwe morali ya kufanya vizuri mechi ijayo.”