Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi kuelekea mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.
“Huu ni mchezo wa fainali, unapaswa kuwa makini sana, nakumbuka vyema mchezo uliopita pale Zanzibar, tayari tunayo picha sahihi tunapaswa kwenda na mbinu gani dhidi ya Azam Fc, niwahakikishie Yanga Sc ni timu imara sana, ukitazama mchezo uliopita Simba walitengeneza nafasi moja tu kwa sababu tulikuwa imara kwenye kila idara.”
“Tutacheza mchezo wetu kama ambavyo tumekuwa tukicheza mara kwa mara, jambo la muhimu ni kuhakikisha hatufanyi makosa madogo madogo, hatupaswi kuruhusu bao kwenye mchezo huu, jambo zuri ni kuwa timu yangu inacheza zaidi kitimu.”