“Klabu yetu haina boss wa kitengo cha habari na mawasiliano,mimi ndio boss wa mawasiliano wa klabu na si mtu mwengine. Klabu tuna afisa habari ambae ndie Ally Kamwe.”
“Klabu inamtambua Ally Kamwe kama afisa habari kwasababu mpaka sasa mkataba wake unasema hivyo. Haji Manara alikuwa Afisa habari wetu na alifanya kazi nzuri sana katika muda wake na alipopata changamoto akafungiwa kama klabu tulihitaji mtu wa kuisemea klabu na hapo ndipo tulimchukua Ally Kamwe.
Kwa sasa Ally kamwe ndie Afisa habari wetu na upande wa Manara yeye ni mwanachama wetu na tunaangalia ni sehemu gani ambayo tutamuweka kwenye klabu”
Eng. Hersi Said, Rais wa klabu ya Yanga