Coastal Union

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Coastal Union zinaeleza kuwa fedha ambayo klabu ya Simba iliingiza kwenye ‘account’ ya Coast Union kwaajili ya biashara ya mchezaji wao, Lameck Lawi zimerudishwa mwenye ‘account’ ya Simba baada ya biashara hiyo kwenda tofauti na makubaliano ya pande zote mbili.

Moja kati ya watu wa ndani wa klabu ameeleza kuwa Simba walipewa tarehe ambayo walipaswa kufanya malipo ya shilingi milioni 205 ambazo ni fedha za usajili wa mchezaji huyo.

Inaelezwa kuwa siku moja kabla ya tarehe husika kufika Simba walipigiwa simu na kusema kuwa wataweka fedha hizo lakini tarehe ilifika na Simba ikawa haijafanya malipo, baada ya muda kupita Simba ilianza kufanya malipo kidogokidogo lakini Coastal waliandika barua ya kusitisha dili hilo kisha wakawarudisha Simba fedha zao zote walizowawekea.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here