Azam Fc

Azam FC watapata Kiasi Cha €200,000 ambayo inafika €220,000 Plus Bonuses ambayo ni sawa 619,323,099.78

Lakini pia Azam FC wameweka Kipengele Cha First Refusal kwa maana kama akitaka Kurejea tena Tanzania Azam wanatakiwa kutaarifiwa kwanza kama Wana uhitaji nae au sio ndo anaweza kwenda team nyingine.

Hii inaonekana ni Biashara nzuri Kwa Azam FC kwasababu Kipre Jr alikuwa amebakisha Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake.

Maana yake Mwezi January Kipre Jr alikuwa anabakisha Miezi 6 kwenye Mkataba wake ambayo ingewaweka kwenye hatari ya Kumpoteza bure.

Baada ya Mazungumzo ya Kuongeza Mkataba na Kipre Jr kuvunjika Azam FC ni kama walianza Kujiandaa na Maisha bila yeye Kwa kumsajili Frank Tiesse kutoka Stade Malien ya nchi Mali.

Msimu uliopita Kipre Jr Alifunga Goli 9 na Kusaidia Goli nyingine 9 kufungwa

Kipre Jr amehusika kwenye goli 18 nyuma tu ya Feisal Salum na Stephanie Aziz

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here