LIGI Kuu Tanzania Bara mzunguko wa pili kasi yake inazidi kuwa kubwa ambapo ni muda wa kukamilisha hesabu.
Mei 8 kuna timu zitakuwa kazini kusaka pointi tatu ndani ya uwanja katika dakika 90 za kazikazi.
Ni Mashujaa watakuwa Uwanja wa Lkae Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma kukabiliana na KMC.
Ikumbukwe kwamba Mashujaa imetoka kupoteza mchezo wake uliopita ikiwa hapo kwa kushuhudia ubao ukisoma Mashujaa 0-1 Yanga.
Mchezo mwingine ni Yanga dhidi a Kagera Sugar huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.
Katika mchezo wao uliopita wa mzunguko wa kwanza Yanga iligawana pointi mojamoja na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.