MATAJIRI wa Dar Azam FC leo Mei 3 2024 wanakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa CRDB Federation dhidi ya Namungo FC.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex ikiwa ni hatua ya robo fainali saa 2:300 usiku kwa wababe hao wawili kusaka ushindi kwa timu itakayotinga hatua ya nusu fainali.
Tayari kwenye robo fainali iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex Yanga waliibuka wababe mbele ya Tabora United kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United hivyo Yanga itacheza nusu fainali na Ihefu.
Bruno Ferry Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri.
“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wetu kwenye mechi ambazo tumekutana nao wamekuwa wakionyesha ushindani hivyo hilo tunalitambua na tupo tayari.
“Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo kwenye mchezo wetu, wachezaji wapo tayari tunaamini kwamba tutapata matokeo mazuri,”.
Shadrack Nsajigwa, kocha msaidizi wa Namungo amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata matokeo.