Mike Tyson

Kupanga ni kuchagua, ndicho alichowahi kukifanya bingwa wa ngumi duniani Mike Tyson kukaa miaka mitano bila ya kufanya mapenzi ili kulinda nguvu zake.

Unajua ilikuwaje? Iki hivi, mabondia duniani wanaamini kufanya mapenzi kunamaliza nguvu mwilini, hivyo wapo wanaokaa miezi mitatu hadi sita wakiwa wanajiandaa na pambano.

Sasa Tyson wakati anataka kuja kuwa bondia wa kulipwa na kuutafuta ‘ustaa’ akaamua kukaa miaka mitano bila kufanya mapenzi kuanzia mwaka 1981 hadi 1986 kwa ajili ya kutunza nguvu, baada ya hapo kilichofuata ni kuwakalisha mabondia kila kukicha.

Miongoni mwa mabondia ambao wanaamini kufanya mapenzi kunapunguza nguvu ni pamoja na Manny Pacquiao na Amir Khan.

Tuambie wewe unaweza kukaa muda gani bila ya kufanya mapenzi?

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here