KWA nyakati tofauti miamba wawili eneo la ushambuliaji Adam Adam na Relliat Lusajo walikuwa katika rada za Simba lakini mipango ikagoma.

Adam aliibukia ndani ya Mashujaa na Lusajo alibaki Namungu kisha dirisha dogo ni mali ya Mashujaa.

Ikumbukwe kwamba Lusajo alipokuwa Namungo aliwahi kuwatungua Simba mzunguko wa kwanza katika Ligi Kuu Bara Uwanja wa Uhuru mwisho ikawa Simba 1-1 Namungo, msimu wa 2023/24.

Nyota hao wawili walikuwa sehemu ya mchezo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Aprili 9 2024 wakati ubao ukisoma Mashujaa 1-1 Simba kwenye dakika 90.

Katika mapigo ya penalti ilikuwa Mashujaa 6-5 Simba ambapo ni Eric Johora kipa wa Mashujaa alikuwa shujaa kwenye mchezo huo na mwamba Adam Adam alifunga moja ya penalti katika hizo sita wakati langoni alipokuwa ni Ally Salim.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here