BURUDANI

RAYVANNY:NAFANYA KAZI USIKU NA MCHANA

Msanii wa Bongo fleva Raymond Shaban ‘Rayvanny’ amesema tuzo alizoshinda anastahili kwasababu halali anafanyakazi usiku na mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari Uwanja wa Ndege Julius Nyerere Rayvanny amesema amezoea kushinda tuzo ila sio tuzo tano.

‘’Nimezoea kushinda tuzo lakini sio tuzo tano kwa wakati mmoja tena za nje ya nchi yangu kwakeli kwangu hii ni kubwa sana.

“Hamna kazi rahisi, kupata tuzo ni kazi sana nilichoshinda kafatilie kwa namna gani tunajituma, nahangaika naruka na ndege masaa 16,13,7, 8 tuzo hizi nastahili kutokana na utendaji wangu wa kazi nafanya kwa bidii” amesema Rayvanny na kuongeza

“Wenyewe mashaidi kila siku nazunguka kila siku sehemu mbalimbali kutafuta collabo na kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti silali usiku na mchana wengine wamelala tu nyumbani.’’ ’’amesema Rayvanny.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button