Mashujaa imechapwa na coastal

Mashujaa FC wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma. imepokea kipigo kutoka kwa Coastal Union kipigo cha  mabao 2-1.

Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Shedrak Malungwe dakika ya 10 na Bakari Selemani dakika ya 57 huku Mashujaa ilipata bao dakika ya 45 lililofungwa na Omari Omari.

Matokeo hayo yameifanya Coastal Union kumesalia nafasi ya nne na pointi 33 huku Mashujaa ikibaki nafasi ya 12 na pointi 21.

Mchezo mwingine ni kati ya Tanzania Prisons na KMC uliomalizika kwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Sare hii imeifanya timu zote mbili kufikisha pointi 29 na kusalia katika nafasi iliyokuwepo awali kabla ligi haijasimama kwa mwezi mzima kupisha mechi za kimataifa za timu za taifa kwa kalenda ya Fifa na michezo ya Kombe la Shirikisho nchini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here