Simba

UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba upo tayari kwa mchezo wao wa raundi ya nne dhidi ya Mashujaa ya Kigoma mwisho wa reli kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.

Ni Aprili 8 mapema Simba waliwasili salama Kigoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Aprili 9 2024 saa 10:00 jioni na yule atakayepoteza ndani ya dakika 90 safari yake itakuwa imegotea hapo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kwamba wanatambua ugumu wa mashindano hayo hasa hatua za mtoano kwa kuwa ni lazima kushinda na sare sio matokeo yanayohitajika.

“Kwenye mashindano haya ya mtoano ambacho kinahitajika ni ushindi na sio sare kwa kuwa ili kusonga mbele hatua inayofuata ni lazima kupata ushindi hakuna chaguo lingine.

“Tunawatambua Mashujaa wao walikuwa na muda wakutusubiri sisi wakati sisi tulikuwa kwenye safari na mechi za kimataifa hivyo kuna utofauti na tunawaheshimu wapinzani wetu kwa namna yoyote ile mchezo utakuwa ni mgumu,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here