MTIBWA Sugar

MTIBWA Sugar wamesepa na pointi tatu mazima dhidi ya Singida Fountain Gate, ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Singida Fountain Gate 0-2 Mtibwa Sugar.

Ushindi wa Mtibwa Sugar umevuruga mipango ya Singida Fountain Gate kukomba pointi tatu kwenye mchezo huo.

Abdul Hilary dakika ya 70 kwa mkwaju wa penàlti na Omary Marungu dakika ya 76 alipachika bao la pili.

Mechi tano Singida Fountain Gate imepoteza nne na kuambulia sare moja.

Mashujaa walikula korosho zote kwa ushindi wa bao 1-0 Namungo, Uwanja wa Lake Tanganyika, wakikomba pointi tatu mazima.

Singida Fountain Gate ni pointi 21 nafasi ya 8, Mtibwa Sugar nafasi ya 16 pointi 12 kibindoni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here