KITAIFA

MSUVA AJIVUNIA KIWANGO CHAKE AFCON

Mchezaji wa Tanzania, Simon Msuva amesema ingawa Taifa Stars wametolewa kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ila yeye anajivunia kiwango alichokionyesha kwenye mashindano hayo kwani yamemuwezesha kupata Timu ya Saudi Arabia ya Al Najmah FC ya Ligi daraja la kwanza

“Tumeshindwa kuingia hatua inayofuata lakini kuna mabadiliko na tutajipanga katika mashindano yajayo, kingine ni kwamba michuano hii imesaidia kupata timu. Sikutaka kukata tamaa na unajua nimetoka kwenye matatizo kwenye timu yangu (JS Kabalie) ya Algeria lakini nilijua tu siwezi kukosa timu ya kuichezea na kweli nimepata hii”

Tanzania imetolewa katika Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON baada ya kupata sare mbele ya DR Congo, Sare iliyoifanya ifikishe alama mbili ikishika mkia huku matokeo hayo yakiwa na faida kwa Congo baada ya kufikisha alama tatu na kuwa nafasi ya pili ambayo imewawezesha kwenda mbele kwenye hatua ya 16 bora.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button