MUDA mchache baada ya  kuachwa kwa winga, Jesus Moloko na Yanga kwenye dirisha hili la usajili kupisha usajili mpya winga huyo amekiri hilo.

Yanga imeachana na winga huyo baada ya kuitumikia kwa misimu miwili hivyo ameungana na Wacongo wenzake Djuma Shaban, Yanick Bangala, Heritier Makambo, Chico Ushindi ambaye hakuweza kuendana na kasi ya Yanga na Fiston Mayele aliyeuzwa nje.

Akizungumza na kunukuliwa na gazeti la Mwanaspoti, Moloko alisema ni kweli amemalizana na Yanga na anatarajia kuondoka nchini kesho kwenda Congo kwa ajili ya maisha mengine mapya ya soka.

“Ni kweli nimepewa barua ya kuachana na Yanga na natarajia kwenda Congo kesho nawashukuru viongozi na mashabiki wa timu hii kwa maisha niliyoishi nao nikiwa ndani ya timu hiyo;

“Nilikuwa na misimu mitatu mizuri na Yanga nimeishi vizuri na wachezaji wenzangu, viongozi na hata mashabiki nawatakia kila la kheri kwenye mashindano wanayoshiriki ndani na nje,” alisema

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here