Author: Chikao

HUKU wengi wakiipa nafasi zaidi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga Machi 30, mwaka huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, ameichambua timu hiyo na kusema hakuna lisilowezekana kwa kuwa watakuwa 11 kwa 11 uwanjani na si vinginevyo. Akiwachambua wapinzani wao hao, Gamondi amesema ubora wa kikosi na bajeti ya usajili wa Mamelodi Sundowns tofauti na Yanga, lakini hilo haliwapi woga, badala yake wanahitaji kupambana na kuweka juhudi zaidi katika mchezo huo wa nyumbani. Gamondi amesema anafahamu misingi ya Mamelodi kwa sababu timu yake ya zamani na wamekuwa…

Read More

WAKIWA na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, Waarabu wa Misri uongozi wa Simba umebainisha kuwa kambi yao itakuwa Zanzibar kwa maandalizi. Timu hiyo inaiwakilisha Tanzania kwenye anga la kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wao wa hatua ya robo fainali unatarajiwa kuchezwa Machi 29 Uwanja wa Mkapa. Mshindi kwenye mchezo wa kwanza atakuwa ametanguliza mguu mmoja hatua ya nusu fainali ambayo itaamuliwa kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza itakayochezwa Misri. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa watakuwa kwenye kambi maalumu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrka dhidi…

Read More

SERIKALI imesaini mkabata wa ujenzi wa Uwanja wa Samia Suluhu Hassan utakaojengwa jijini Arusha na kugharimu Sh bilioni 286. Akishuhudia utiaji saini, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema dhumuni la kujenga uwanja huo jijini Arusha ni kwaajili ya kuchochea maendeleo ya sekta ya utalii kupitia michezo. Ujenzi wa uwanja huu ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu mwenyeji wa michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2027. Mataifa mengine ni Kenya na Uganda.

Read More

BAADA ya kupoteza pointi tatu mbele ya Azam FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amemtupia lawama kwa waaamuzi wa mchezo huo akidai wameruhusu bao la pili ambalo inaonyesha kuwa mfungaji alikuwa ameotea. Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji Feisal Salum ‘Fei Toto’, dakika ya 51, Yanga ilipoteza pointi tatu mbele ya Azam FC kwa kukubali kichapo cha mabao 2_1, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam. Gamondi amesema mechi ilikuwa ya ushindani mkubwa na kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kushindwa kutumia nafasi zilizopatikana. Amesema wamefanya makosa katika boksi lao la Azam…

Read More

Simba inarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, huku kocha wa zamani wa timu hiyo, Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akilianika faili zima la waarabu akisema anawajulia ndio maana hawakumfunga walipokutana kwenye AFL. Wekundu wa Msimbazi walikutana na Al Ahly katika mechi mbili za michuano mipya ya Africans Football League ikiwa chini ya Robertinho na kutoka sare ya mabao 3-3, zikifungana 2-2 nyumbani kisha 1-1 ugenini na Wamisri walisonga mbekle nusu fainali kwa kanuni ya mabao mengi ya ugenini. Timu hizo zitakutana tena katika mechi za robo fainali ya…

Read More

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa mpango mkubwa kwa sasa  ni kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri. Timu hiyo imetinga hatua hiyo ikiwa nafasi ya pili kwenye kundi B na pointi zake ni 9 inatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa kwanza nyumbani, Uwanja wa Mkapa. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa mpango mkubwa kutinga hatua ya nusu fainali ni muhimu kupata matokeo dhidi ya Al Ahly katika robo fainali. “Sasa tunaanza maandalizi rasmi ya mchezo wetu wa robo fainali dhidi ya Al Ahly. Kwenye Makundi yetu ya WhatsApp na matawi yetu tuanze kuhamasishana tujitokeze kwa wingi…

Read More

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamekomba pointi tatu mazima kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Azam FC 2 -1 Yanga. Mabao ya yamefungwa na Feisal Salum dakika ya 51 na Gibril Sillah dakika ya 19 kwa Azam ni Clement Mzize kwa Yanga dakika ya 10. Mzunguko wa pili ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo ule wa kwanza ni Yanga walikomba pointi tatu. Kwenye mchezo wa Machi 17 2024 kadi 7 za njano zimetolewa huku Azam FC wachezaji wanne na Yanga wachezaji watatu walionyeshwa Kadi za njano na mwamuzi wa kati. Pacome Zouzoua alipata maumivu na…

Read More

SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa Simba ameweka wazi kuwa ligi inakwenda ukingoni jambo ambalo linaongeza nguvu kwa kila timu kupambana kupata matokeo. Timu hiyo kwenye mechi tatu zilizopita ilipata ushindi katika mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Jamhuri. Machi 15 2024 watakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mashujaa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex. Kocha huyo amesema; “Kwa sasa ligi inakwenda ukingoni kila timu inapambana kupata matokeo mazuri ili kufikia malengo yake kwa kujiondoa kutoka nafasi ambayo ipo. “Tunatambua ushindani ni mkubwa nasi tunafanya maandalizi mazuri kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza tupo tayari,”. Mchezo uliopita ubao wa…

Read More

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema wanatambua mchezo dhidi ya Geita Gold hautakuwa mwepesi licha ya kuwa na mwendo mzuri katika mechi zilizopita. Kocha huyo amebainisha kwamba hawezi kusema kwamba watafunga mabao mengi kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold kwa kuwa yeye hafanyi kazi ya ubashiri. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku ikiwa ni mzunguko wa pili,ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Yanga ilikomba pointi tatu. Gamondi amesema:”Tumejiandaa vizuri kucheza na Geita Gold, tunafahamu kila mpinzani kuna namna yake ya kujiandaa kimbinu, Ukitazama matokeo yao ya hivi karibuni wameimarika hivyo lazima tuchukue tahadhari ya kutosha…

Read More