Aliyekuwa mlinda lango wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa Hispania David De Gea baada ya mwishoni mwa juma lililopita kujiunga na klabu ya Fiorentina akiwa mchezaji huru hatimaye ameanza rasmi mazoezi kwaajili ya msimu mpya wa loigi kuu Italia.
De Gea mwenye umri wa miaka 33 alilazimika kukaa nje ya msimu kwa karibu msimu mzima mara baada ya kuachwa na Manchester United msimu juzi baada ya mkataba wake kumalizika na kumpisha kipa wa Cameroon Andre Onana.
De Gea aliachwa na United msimu ambao aliibuka kuwa kipa bora wa msimu wa ligi kuu Uingereza 2022-23.