FEI TOTO KUSAJILIWA SIMBA? AHMED ALLY AFUNGUKA HAYA
Je Fei Toto Kusajiliwa Simba?
Moja kati ya shauku kubwa ya mashabiki wa msimbazi ni kusikia neno fei toto kusajiliwa simba na hii ni kutokana na kuwa na uhitaji wa mchezaji mwenye kariba yake katika kipindi hiki cha kuimarisha kikosi, Afisa habari wa klabu ya simba Ahmed Ally amesema.
“Feisal Salum jina lake nalisikia sikia sana akihusishwa na Simba SC ni mchezaji mzuri ambae kusema kweli ambae mimi mwenyewe ndoto yangau ni kuja kufanya kazi na Feisal Salum ndani ya Simba”.
“Kwahiyo ni aina ya mchezaji ambae kusema kweli kila mtu anatamani akitumikia timu yake lakini kwa sasa ni mchezaji wa Azam FC na mimi sijapata maelekezo yoyote kwamba tumefungua meza ya mazungumzo na Azam FC kuhusiana na Feisal Salum”.
Ahmed Ally Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC