Duchu kuondoka Simba

SIMBA huenda ikamtoa kwa mkopo beki wake wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ baada ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa msimu uliopita.

Inaelezwa kwamba Simba na Duchu wapo kwenye mazungumzo na timu nyingine za Ligi Kuu Bara ili kumpeleka beki huyo ambaye awali alitua kikosini hapo Agosti 2020 akitokea Lipuli ya Iringa.

Katika eneo lake ndani ya Simba amekuwa akicheza Shomari Kapombe na wakati mwingine Israel Mwenda, huku yeye akisugua benchi.

Hata hivyo zipo timu tatu ambazo zinatajwa kwa sasa kumtaka mchezaji huyo, ikiwamo Pamba Jiji ambayo imepanda msimu huu ikitokea Championship msimu uliopita.

Timu nyingine ni KenGold na Singida Fountain Gate, lakini hadi jana asubuhi kulikuwa hakuna ambayo ilikuwa imemalizana na Simba wala mchezaji huyo.

Hadi sasa Simba imefanya usajili wa wachezaji wa Kimataifa pekee wapya, 11 huku wakibakiza nafasi moja kumamilisha idadi inayohitajka ya wachezaji wa kigeni.

Simba imewasajili kwa dau kubwa zaidi msimu huu wachezaji wafuatao, Joshua Mutale, Jean Charles Ahoua, Steve Mukwala, Augustine Okejepha, Chamou Karaboue, Deborah Ferndandes, Valentine Nouma.

Wachezaji wa zamani ni Ayub Lakred aliyeongeza mkataba, Che Fondoh Malone, Fabrice Ngoma, na Freddy Michael Kaublan.

Hadi sasa Simba imeachana na wachezaji wakubwa kadhaa ikiwemo Clatous Chama ambaye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya hayakufanikiwa, na akajiunga na Ynaga, Saidoo Ntibazonkiza, Henock Inonga aliyeuzwa, Luis Miquissone John Bocco na Kennedy Juma.

Huku majina mengine kama Babacar SAR, Sadio Kanoute, Par Omar Jobe, Willy Esomba Onana, Aubin Kramo yakiwekwa kwenye mabano muda wowote yatatanazwa kuachwa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here