ULE mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki Bongo Mzizima Dabi umepangiwa tarehe na sasa siku zinahesabika kufika muda wa wababe wawili kusaka ushindi.
Ni Mzizima Dabi inatarajiwa kuwa Mei 9 kwa wababe wawili Azam FC kumenyana na Simba.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-1 Azam FC.
Bao la Simba lilifungwa na Clatous Chama na bao la Azam FC lilifungwa na mwamba Prince Dube.
Kazi itakuwepo kwa wababe hao wawili kwa kuwa kila mmoja anapambania kupata pointi tatu mbele ya mpinzani wake.