Coastal Union

POINTI moja waliyovuna kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons inawabakisha Coastal Union kwenye nafasi ile ya nne.

Mei 6 2024, Coastal Union ilikuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 0-0 Tanzania Prisons hivyo wababe hao wote wawili waligawana pointi mojamoja.

Ni pointi 34 wanafikisha Coastal Union nafasi ya nne kwenye msimamo huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya sita na pointi 32 kibindoni.

Ipo wazi kwamba vinara wa ligi ni Yanga weye pointi 65 baada ya kucheza mechi 25.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YA SOKALEO, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here